Wazazi wa Diamond waumwa hoi.....

      Wazazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim na Abdul Juma wako hoi vitandani wakikabiliwa na maradhi mbalimbali
     

MAMA DIAMOND

Mama Diamond hajiwezi kwa mwezi mmoja sasa akisumbuliwa na maradhi yenye kuashiria kupooza sehemu ya mwili na kushindwa kutembea. Anaugulia nyumbani kwake, Sinza ya Mori jijini Dar es Salaam.

DAKTARI ASHAURI

Kwa mujibu wa daktari mtaalamu wa viungo, alishauri kuwa endapo mama Diamond amepooza ni vyema akapata tiba kwa wataalamu wa viungo mapema kwani tatizo linaweza kuongezeka.

Bi. Sanura Kasim akiwa hoi kwa ugonjwa.

BABA DIAMOND

Chanzo hicho kilieleza kuwa, baba Diamond kwa muda mrefu usiorekodiwa siku, anasumbuliwa na maumivu makali ya miguu, naye kwa kiasi cha kushindwa kutembea.
“Yeye anaugulia mafichoni kwani ndugu zake wamemficha mahali pasipojulikana ili watu wasimwone. Inaaminika kuna mambo ya kishirikina ndani yake,” kilisema chanzo hicho bila kufafanua ushirikina wa vipi!


 
Baba wa 'Diamond Platnumz', Abdul Juma.

No comments:

Post a Comment