
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli Hayyat Regency Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung,Mike Seo amesema kuwa, "kwa kutambua ongezeko la uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora kuwasiliana na wateja wetu kupitia mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana na vifaa vyetu na soko letu.
Amesema "Tunafuraha sana kutangaza ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi tunafuraha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu. "
Seo amesema mkataba wa Vanessa na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara tosha ya makubaliano rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho kilihashiria mwanzo wa kazi mpya kama mwakilishi wa kampuni ya Samsung.
Akiwa kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo.
Kwa upande Vanessa amesema furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung, binafsi, natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania,Mike Sio (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwanamuziki Vannesa Mdee kuwa Balozi wa Kampuni hiyo.
Kulia ni Meneja wa Mwanamuziki Vannesa Mdee,Michele Baldin.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania,Mike Sio (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Samsung Tanzania,Vannesa Mdee (pili kushoto), Meneja wa Mwanamuziki Vannesa Mdee,Michele Baldin (kushoto) pamoja na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni hiyo,Sylvester Manyara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania,Mike Sio akimuonyesha kitu kwenye simu ya Samsung Balozi wa Samsung Tanzania,Vannesa Mdee mara baada ya kusaini mkataba.
No comments:
Post a Comment