maswali 10 ‘hot’ aliyoulizwa staa wa bongo movie Vanitha Omary na yeye kutoa ushirikiano katika kuyajibu licha ya kwamba aliachwa kijasho chembamba kikimtoka
mahojiano yalikuwa hivi:
paparazi: Kuna hizi tetesi kwamba huyu mume wako wa sasa alikuwa ni mpenzi wa rafiki yako Joan Matovolwa lakini wewe ukampora na mkaishia kuoana, hili unalizungumziaje?
Vanitha: (Kicheko) Ukweli ni kwamba mimi na Joan ni marafiki wakubwa na hilo unaloongea halina ukweli wowote. Maneno hayo yaliibuka baada ya kuwepo taarifa kuwa nataka kuolewa.
paparazi: Wewe ni msanii lakini ni mke wa mtu, siku ukiwa hujaenda kwenye shughuli zako za kisanii uwapo nyumbani huwa unafanya nini?
Vanitha: Huwa napenda kupikapika.
paparazi:Wewe ni mke wa mtu halafu ni msanii, je unapokuwa nyumbani unapenda kumpikia chakula gani mumeo?
Vanitha: Nikiwa nyumbani napenda kumpikia baby wangu chakula kizuri ambacho ni kipya.
paparazi: Je, pale unapokuwa faragha na mumeo unapenda kumtega kwa vivazi gani?
Vanitha: Ukweli huwa simtegi kwa mavazi, napenda kumtega kwa kukaa mtupu kwani wakati huo huwa ni wake, kwa nini nimfichie mali zake?
paparazi: Ni upi ugonjwa wako uwapo faragha na huyo mumeo?
Vanitha: Napenda sana kumkumbatia na yeye anikumbatie. Kale kajoto kanakotokea huku tukinong’onezana maneno matamu mimi nabaki kusinziasinzia.
paparazi: Watu wanasema wanaume hawatabiriki kwa kuchepuka, hivi siku ukimfumania mumeo utafanya nini?
Vanitha: Naomba Mungu isitokee kwani nahisi nitafanya tukio baya na kumuacha siwezi, dah! Nahisi kutetemeka ukiniambia hivyo.
paparazi: Mastaa wana skendo ya kuchukua waume za watu, wewe unamlindaje mumeo asinaswe na wezi hao?
Vanitha: Siwezi kusema nitamlinda kwani sijui mtu anakuwa na nia gani na atakuwa amejipanga vipi ila nabaki kumuomba Mungu amuepushe mume wangu na vishawishi.
paparazi: Kuna wanawake ambao eti wanaona kuwapa waume zao mapenzi kinyume na maumbile ndiyo kuwashika, wewe kwako likoje hili?
Vanitha: Mungu aniepushie mbali kwani ni jambo baya sana, sijawahi na sitowahi, nawaomba wanaofanya hivyo kuacha kwani Mungu hapendi.
paparazi: Ni kitu gani kimewahi kukufurahisha katika maisha yako?
Vanitha: Nilifurahi sana siku niliyofunga ndoa na mume wangu kwani tulipitia mikikimikiki mingi. Tumekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.
paparazi: Siku uliyohuzunika sana unaweza kuikumbuka?
Vanitha: Ni siku bibi yangu alipofariki, nakumbuka nilikuwa katika wakati mgumu kwani yeye ndiye alikuwa mlezi wangu na nilikuwa na ujauzito.
paparazi: Mbali na sanaa, ni kazi gani unaifanya?
Vanitha: Mimi ni mbunifu wa kupamba nyumba, nafanya kazi ya kuwadizainia watu nyumba zao kwa mapambo mpaka muonekano mzima wa nyumba .
No comments:
Post a Comment