Jamaa huyu hakuwa anafahamika sana hata kwenye matamasha mbalimbali ulikuwa huwezi kumkuta lakini baada ya kupata kazi ya kumlinda staa wa Bongo Flava nchini Naseeb Abdul "Diamond" alianza kujulikana zaidi huku watu wakimchukulia kama mtu wa kawaida sana kama mabaunsa wengine. Jina lake harisi anaitwa Mwarabu Suleiman Mirundi huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii.kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana huwezi kumkuta mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani.
akiwa mazoezinii Mwarabu Suleiman Mirundi
.jpg)
Bodigadi wa Diamond Mwarabu Seleman Mirundi akifanya mazoezi ya kikomandoo kwenye msitu wa chuo kikuu kuhofia watu wasione mazoezi yake
Baada ya kutonywa sehemu anapoweza kupatikana kijana huyo ambapo ni msitu wa chuo kikuu ndiko anakofanyia mazoezi mara nyingi akiwa na mwanamuziki na bondia Zora D ndipo nilipofunga safari hadi huko na kumkuta kijana huyo akifanya mazoezi ya hatari kuyaona. Mwarabu alianza kuelezea ingawa hakupenda watu wajue kama yeye ni mtu wa aina hiyo lakini alianza kufunguka kama ifuatavyo " mimi ni Komandoo lakini sio wa JWTZ hapana nimefuzu mazoezi haya ya mapigano nchini Iran toka mwaka 2010 baada ya kwenda kule kuchgeza mchezo wa kutumia mabavu ndipo niliposhinda kwa kumchakaza vibaya Komandoo wa Iran" Alisema Mwarabu Baada ya hapo Jeshi la nchi hiyo baada ya kumuona sio mtu wa kawaida kuwa raia wa kawaida ndipo alipochukuliwa Kambini humo kwaajili ya kufanya mazoezi hayo ya hatari duniani hadi mwaka juzi 2013 ndipo walipompatia cheti cha kuhitimu kama kinavyoonekana pichani. Hata hivyo Mwarabu anasema kwa jinsi alivyo na mazoezi aliyoyapata chini ya watu kumi hatakiwi kupigana nao hata wakija na shoka isipokuwa zaidi ya hapo ndipo kidogo atawapiga makofi tu na kuwaacha lakini sio aseme atoe kichapo kwani pigo lake moja mtu anabadilishwa jina mara moja na kuitwa marehemu. Mwarabu ambae kwa sasa ameajiriwa na mwanamuziki Diamond na analipwa mshara mnono kwa kazi ya kumlinda ambapo hadi sasa amenunua viwanja kadhaa na ujenzi unaendelea na si nyumba za kitoto huku akiwa na usafari zaidi ya gari tatu ambapo moja boss wake alimnunulia na mbili amenunua kwa mshahara anaomlipa na hadi sasa anakafikisha kilo 190 wastani wa kilo 200. Lakini pia bodigadi huyo ambae pia ameshiriki filamu ya Expendables ya Tanzania ya msanii Manaiki Sanga ambae kabla ya kutua kwa Diamond aliwahi kumlinda Manaiki Sanga.
.jpg)
Mwarabu akifanya mazoezi mepesi na mmoja ya watu muhimu nchini
.jpg)
akiwa katika mazoezi makali
.jpg)
Hiki ni chetu alichotukiwa nchini Iraq baada ya kumsambaratisha
Komandoo wa nchi hiyo ambae hakumtaja jina.
Hiki pia cheti alichotunukiwa na nchini Mozambique baada
ya kuwatandika wanajeshi kadhaa nchini humo
Mwarabu Seleman Mirundi akiwa nyuma ya bendera ya Tanzania tayari kupambana na Komandoo wa Iran ambae hata hivyo alimchakaza vibaya na kuokolewa raundi ya kwanza
Hapa Mwarabu akiwajibika kumlinda boss wake nchini Burundi.
ina lake harisi anaitwa
Mwarabu Suleiman Mirundi huyu maskanibongotz baada ya kupata taarifa za
kuwa huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii ilifanyajitihada za
kumtafuta huku kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana huwezi kumkuta
mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani. Copy and
WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
ina lake harisi anaitwa
Mwarabu Suleiman Mirundi huyu maskanibongotz baada ya kupata taarifa za
kuwa huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii ilifanyajitihada za
kumtafuta huku kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana huwezi kumkuta
mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani. Copy and
WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment