Hakika za mwizi 40,majambazi yakamatwa Zanzibar.......

       Majambazi wamekamatwa Darajani Zanzibar jana baada ya kufyatuliana risasi na polisi wakati wakijaribu kukimbia. Katika tukio hilo wananchi kadhaa walijeruhiwa kwa kugongwa na gari katika harakati za majambazi hayo kukimbia. Polisi imewatia mbaroni majambazi watatu baada ya wananchi kutoa ushirikiano.
 

Mmojawapo ya majambazi waliokamatwa akiwa hoi baada ya kujeruhiwa na polisi.

  

 

Jambazi huyo akiwa katika gari la polisi.

 

mmoja wa watuhumiwa wa ujambazi akiwa chini ya ulinzi wa polisi.. 

Wazazi wa Diamond waumwa hoi.....

      Wazazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim na Abdul Juma wako hoi vitandani wakikabiliwa na maradhi mbalimbali
     

MAMA DIAMOND

Mama Diamond hajiwezi kwa mwezi mmoja sasa akisumbuliwa na maradhi yenye kuashiria kupooza sehemu ya mwili na kushindwa kutembea. Anaugulia nyumbani kwake, Sinza ya Mori jijini Dar es Salaam.

DAKTARI ASHAURI

Kwa mujibu wa daktari mtaalamu wa viungo, alishauri kuwa endapo mama Diamond amepooza ni vyema akapata tiba kwa wataalamu wa viungo mapema kwani tatizo linaweza kuongezeka.

Bi. Sanura Kasim akiwa hoi kwa ugonjwa.

BABA DIAMOND

Chanzo hicho kilieleza kuwa, baba Diamond kwa muda mrefu usiorekodiwa siku, anasumbuliwa na maumivu makali ya miguu, naye kwa kiasi cha kushindwa kutembea.
“Yeye anaugulia mafichoni kwani ndugu zake wamemficha mahali pasipojulikana ili watu wasimwone. Inaaminika kuna mambo ya kishirikina ndani yake,” kilisema chanzo hicho bila kufafanua ushirikina wa vipi!


 
Baba wa 'Diamond Platnumz', Abdul Juma.

Mmmh kumbe bodyguard wa Diamond ni komandoo tena aliye fuzu mafunzoo.....


         Jamaa huyu hakuwa anafahamika sana hata kwenye matamasha mbalimbali ulikuwa huwezi kumkuta lakini baada ya kupata kazi ya kumlinda staa wa Bongo Flava nchini Naseeb Abdul "Diamond" alianza kujulikana zaidi huku watu wakimchukulia kama mtu wa kawaida sana kama mabaunsa wengine. Jina lake harisi anaitwa Mwarabu Suleiman Mirundi huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii.kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana huwezi kumkuta mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani.

 

akiwa mazoezinii Mwarabu Suleiman Mirundi



Bodigadi wa Diamond Mwarabu Seleman Mirundi akifanya mazoezi ya kikomandoo kwenye msitu wa chuo kikuu kuhofia watu wasione mazoezi yake


Baada ya kutonywa sehemu anapoweza kupatikana kijana huyo ambapo ni msitu wa chuo kikuu ndiko anakofanyia mazoezi mara nyingi akiwa na mwanamuziki na bondia Zora D ndipo nilipofunga safari hadi huko na kumkuta kijana huyo akifanya mazoezi ya hatari kuyaona. Mwarabu alianza kuelezea ingawa hakupenda watu wajue kama yeye ni mtu wa aina hiyo lakini alianza kufunguka kama ifuatavyo " mimi ni Komandoo lakini sio wa JWTZ hapana nimefuzu mazoezi haya ya mapigano nchini Iran toka mwaka 2010 baada ya kwenda kule kuchgeza mchezo wa kutumia mabavu ndipo niliposhinda kwa kumchakaza vibaya Komandoo wa Iran" Alisema Mwarabu Baada ya hapo Jeshi la nchi hiyo baada ya kumuona sio mtu wa kawaida kuwa raia wa kawaida ndipo alipochukuliwa Kambini humo kwaajili ya kufanya mazoezi hayo ya hatari duniani hadi mwaka juzi 2013 ndipo walipompatia cheti cha kuhitimu kama kinavyoonekana pichani. Hata hivyo Mwarabu anasema kwa jinsi alivyo na mazoezi aliyoyapata chini ya watu kumi hatakiwi kupigana nao hata wakija na shoka isipokuwa zaidi ya hapo ndipo kidogo atawapiga makofi tu na kuwaacha lakini sio aseme atoe kichapo kwani pigo lake moja mtu anabadilishwa jina mara moja na kuitwa marehemu. Mwarabu ambae kwa sasa ameajiriwa na mwanamuziki Diamond na analipwa mshara mnono kwa kazi ya kumlinda ambapo hadi sasa amenunua viwanja kadhaa na ujenzi unaendelea na si nyumba za kitoto huku akiwa na usafari zaidi ya gari tatu ambapo moja boss wake alimnunulia na mbili amenunua kwa mshahara anaomlipa na hadi sasa anakafikisha kilo 190 wastani wa kilo 200. Lakini pia bodigadi huyo ambae pia ameshiriki filamu ya Expendables ya Tanzania ya msanii Manaiki Sanga ambae kabla ya kutua kwa Diamond aliwahi kumlinda Manaiki Sanga.

 

Mwarabu akifanya mazoezi mepesi na mmoja ya watu muhimu nchini









akiwa katika mazoezi makali



Hiki ni chetu alichotukiwa nchini Iraq baada ya kumsambaratisha 

Komandoo wa nchi hiyo ambae hakumtaja jina.

 

 

Hiki pia cheti alichotunukiwa na nchini Mozambique baada 

ya kuwatandika wanajeshi kadhaa nchini humo

 

 

Mwarabu Seleman Mirundi akiwa nyuma ya bendera ya Tanzania tayari kupambana na Komandoo wa Iran ambae hata hivyo alimchakaza vibaya na kuokolewa raundi ya kwanza 



Hapa Mwarabu akiwajibika kumlinda boss wake nchini Burundi.

ina lake harisi anaitwa Mwarabu Suleiman Mirundi huyu maskanibongotz baada ya kupata taarifa za kuwa huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii ilifanyajitihada za kumtafuta huku kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana huwezi kumkuta mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani. Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
ina lake harisi anaitwa Mwarabu Suleiman Mirundi huyu maskanibongotz baada ya kupata taarifa za kuwa huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii ilifanyajitihada za kumtafuta huku kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana huwezi kumkuta mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani. Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win